Baada ya kushiriki kikao maalum na Bodi ya ligi (TPLB) kusaka mwafaka wa mchezo namba 184 kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopaswa kufanyika March 08, klabu ya Yanga imesisitiza msimamo wake wa kutocheza Mechi iliyopangwa Juni 15
Taarifa iliyotolewa na Yanga muda mfupi baada ya kushiriki kikao hicho ikiongozwa na Makamu wa Rais Arafat Haji, imebainisha kuwa klabu imesisitiza kutocheza Juni 15 hadi pale madai yao waliyowasilisha kwa Bodi hiyo March 09 yafanyiwe kazi
Yanga imeitakia kila la kheri TPLB na TFF katika kufanyia kazi madai hayo ili kumaliza mgogoro unaohusu mchezo huo
ADVERTISE HERE