Mashabiki watoa maoni, wataka Nsajigwa arudishwe Yanga B, viongozi mmesikia?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 May 2018
Mashabiki watoa maoni, wataka Nsajigwa arudishwe Yanga B, viongozi mmesikia?
Ukweli ni kwamba licha ya mashabiki wa Yanga kufahamu mazingira inayopita timu yao sasa, matokeo ya kutoshinda kwa muda mrefu yameendelea kuwamumiza.

Mara ya mwisho Yanga kushinda mchezo ilikuwa April 07 kwenye uwanja wa Taifa ilipoichapa Wolaitta Dicha kwa mabao 2-0.

Pia huo ndio ulikuwa mchezo wa mwisho kwa aliyekuwa kocha wake George Lwandamina ambaye tangu aondoke Yanga, klabu hiyo haijaonja radha ya ushindi kwenye michezo saba iliyocheza.

Baada ya kuondoka Lwandamina mikoba yake walikabidhiwa Noel Mwandila na Shedrack Nsajigwa ambapo kimsingi Nsajigwa ndiye aliyekuwa akikinoa kikosi licha ya kuwa msaidizi wa Mwandila kutokana na kukosa leseni inayomuwezesha kuwa kocha Mkuu.

Mwandila ana utalaamu zaidi wa mazoezi ya viungo.

Kama kocha mwingine yeyote Nsajigwa hawezi kukwepa lawama anazotupiwa na mashabiki ambao wanataka kuiona timu yao ikifanya vizuri.

Vipigo vitatu mfululizo vya VPL kutoka kwa Simba, Prisons na Mtibwa Sugar bila ya kujali mazingira yake, ni sababu tosha ya mashabiki kuhoji uwezo wake.

Makocha wanaajiliwa ili wafukuzwe pale timu wanazofundisha zinapofanya vibaya.

Sasa kama matokeo hayapatikani sasa ikiwa ni michezo saba imepita, basi ni halali kwa mashabiki kutaka mabadiliko.

Wengi wametoa mapendekezo wakitaka kocha huyo aliyepata mafanikio makubwa wakati akikinoa kikosi cha pili cha Yanga, maarufu (Yanga B), arejeshwe katika timu hiyo na nafasi yake atafutwe kocha mwingine atayesaidiana na Zahera.

Kwa sasa Zahera ndiye kocha Mkuu wa Yanga lakini bado hajaanza majukumu yake rasmi (kiofisi) kwa kuwa bado Yanga iko kwenye mchakato wa kukamilisha vibali vya kumuwezesha kufanya kazi nchini.

Akiwa Yanga B Njasjigwa aliweza kuwaandaa wachezaji kama Yusuph Mhilu, Maka Edward, Said Mussa 'Ronaldo', Ramadhani Kabwili na wengine wengi ambao wamesajiliwa na timu mbalimbali.

Baadhi ya mashabiki wamependekeza kurejeshwa kwa Juma Mwambusi, ambaye hana timu tangu alipoondoka Yanga baada ya mkataba wake kumalizika.

Mwambusi alifanya kazi na Pluijm na Lwandamina katika vipindi tofauti na aliifanikisha Yanga kutwaa mataji mawili ya ligi kuu ya Vodacom.

Mwambusi alitua Yanga baada ya kupendekezwa na Mkwasa wakati alipoteuliwa kuinoa timu ya Taifa mwaka 2015.

Pia wamo Mecky Mexime na aliyekuwa kocha wa Mbao FC Etienne Ndayiragije ambaye alirejea kwao nchini Burundi baada ya kutofautina na uongozi wa Mbao FC.

Jina la Fred Felix Minziro aliyeipandisha ligi kuu KMC msimu huu nalo ni miongoni mwa wanaopendekezwa kurithi mikoba ya Nsajigwa Yanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’