Benki ya CRDB imejibu madai ya Yanga kutolipwa fedha za ubingwa wa kombe la CRDB 2023/24
Kupitia taarifa iliyotolewa na benki hiyo mapema leo, CRDB wamesema walilipa fedha yote msimu uliopita kwa TFF kwa kuzingatia makubaliano ya kimkataba
Hivyo ni wazi TFF ndio wanaopaswa kutoa maelezo kwa nini klabu ya Yanga haijalipwa fedha zake takribani mwaka sasa?

Baada ya taarifa ya CRDB, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kupokea malipo hayo kiasi cha Tsh Milioni 255
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF, fedha za ubingwa (Mil 200) zimetumika kulipa madeni ambayo klabu ya Yanga inadaiwa na TFF
TFF imeeleza kuwasiliana na Yanga itume mtaalam wa mahesabu ya fedha kwa Shirikisho hilo kwa ajili ya kwenda kuhakiki madeni hayo
