Wapinzani wa Yanga kwenye mchezo wa pili wa kombe la Shirikisho, Rayon Sport wanatarajia kuwasili jijini Dar es salaam leo.
Timu hiyo kutoka Rwanda itacheza na Yanga keshokutwa Jumatano May 16 2018 katika mchezo wa kombe la shirikisho kundi D utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Mchezo huo utaanza saa moja kamili jioni.
Rayon ilitoka sare ya bao 1-1 na Gor Mahia kwenye mchezo wa kwanza ikiwa nyumbani wakati Yanga ililazwa mabao 4-0 na USM Alger ugenini.
Yanga imekuwa ikijifua kikamilifu tangu iliporejea kutoka nchini Algeria May 07, inahitaji kushinda mchezo huo ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo yenye 'ukwasi' mkubwa.

ADVERTISE HERE