Yanga yaendelea kujifua KMC Complex, morali ya timu iko juu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jun 2025
Yanga yaendelea kujifua KMC Complex, morali ya timu iko juu

Klabu ya Yanga SC inaendelea na maandalizi makali kwenye dimba la KMC Complex huku ikiweka mkazo mkubwa katika kuhitimisha msimu kwa kishindo.

Ingawa kumekuwa na sintofahamu inayoizunguka mechi ya dabi dhidi ya Simba SC, mvutano huo haujaathiri kwa namna yoyote morali na ari ya kikosi cha kocha Miloud Hamdi.

Kikosi cha Yanga kimeonekana kuwa na umoja na mshikamano mkubwa katika mazoezi, kikilenga kutetea mataji yote mawili yaliyosalia, Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la CRDB.

Nyota wa timu hiyo wanaonyesha kiu ya mafanikio mazoezini, jambo linalodhihirisha kuwa vijana wa Jangwani wamejipanga kufunga msimu kwa nguvu na kulinda makombe yote.

Meneja wa Yanga, Walter Harrison, amesema maandalizi yanaendelea kwa umakini mkubwa bila kuyumbishwa na hali ya sasa ya mvutano kuhusu mchezo wa dabi.

"Tunafanya maandalizi kikamilifu, hatuwezi kuruhusu mambo ya nje ya uwanja yaingilie utayari wetu. Tunapaswa kuwa tayari wakati wowote timu itakapohitajika kushuka dimbani," alisema Harrison kwa kujiamini.

Yanga inatarajiwa kushuka dimbani Juni 18 kuwakabili Tanzania Prisons, kabla ya kuivaa Dodoma Jiji katika mchezo wa mwisho wa msimu.

Hata hivyo, hatma ya michezo hiyo miwili bado ipo kwenye mizani, ikitegemea maamuzi kuhusu mechi ya dabi dhidi ya Simba ambapo endapo masharti ya Yanga hayatatekelezwa, huenda Wanajangwani wakafunga msimu bila kucheza mechi hizo mbili za mwisho.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’