Nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' amewataka mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa keshokutwa Jumatano wakati Yanga itakapokuwa inachuana na Rayon Sports kwenye mchezo wa pili wa kombe la Shirikisho Barani Afrika, kundi D.
Nadir amesema Yanga imefanya maandalizi ya kutosha na imeandaa burudani mbashara kwa mashabiki wake. Kuweza kuishuhudia wafike kwa wingi katika uwanja wa Taifa.
"Timu inahitaji mashabiki na mashabiki wanahitaji timu. Sehemu pekee tunapoweza kukutana ni uwanjani," amesema Nadir.
Yanga itakuwa inasaka ushindi wake wa kwanza kwenye michuano hiyo ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali.
Baada ya kufungwa mabao 4-0 na USM Alger kwenye mchezo wake wa kwanza, ushindi ni matokeo ya lazima katika mchezo dhidi ya Rayon

ADVERTISE HERE