Kuelekea Derby ya Kariakoo inayotarajiwa kupigwa leo Jumatano Juni 25 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, klabu ya Yanga SC itaingia katika pambano hilo la kukata na shoka ikiwa na rekodi ya kihistoria ambayo haijawahi kushuhudiwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara ndani ya kipindi cha miaka 10
Katika mchezo wao wa hivi karibuni dhidi ya Dodoma Jiji FC, Yanga walitakata kwa ushindi mnono wa mabao 5-0. Bao la mwisho katika mchezo huo lilifungwa na Max Nzengeli, na likawa la 81 kwa Yanga katika msimu huu wa 2024/25 na kuweka rekodi mpya ya idadi kubwa ya mabao ndani ya mechi 29.
Katika kipindi cha miaka 10, hakuna timu iliyowahi kufikia kiwango hiki cha ubora na ufanisiΒ mbele ya lango la timu pinzani
Mechi ya kuamua ubingwa
Derby ya kesho si mchezo wa kawaida, ni fainali isiyo rasmi ya Ligi Kuu NBC. Mchezo huu wa mwisho kwa msimu wa 2024/25, utawakutanisha wapinzani wakuu katika mbio za ubingwa:
Katka mchezo huo Yanga SC wanahitaji sare au ushindi ili kutwaa ubingwa wao wa nne mfululizo huku watani zao Simba SC wanahitaji ushindi wa lazima ili kuwa mabingwa
Hali ya mchezo inatarajiwa kuwa ya kipekee, ikizingatiwa historia, ushindani wa jadi kati ya timu hizo, na uzito wa taji linalosubiri mshindi.
Yanga SC wanakwenda Kariakoo Derby wakiwa kileleni mwa msimamo, ari na morali ya juu, na lengo moja tu, kukamilisha kazi na kurejesha taji Jangwani.
Licha ya propaganda zinazofanywa na watani zao Simba ambao leo hawakutokea kwenye Mkutano na wanahabari huku pia kukiwa na taarifa kuwa watakacha mkutano wa mwisho kabla ya mchezo huo 'pre-match meeting', uhakika ni kuwa watakwenda uwanjani siku ya Jumatano
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wanachofanya watani zao ni kujaribu kuathiri mapato ambayo Yanga inaweza kupata kama uwanja utajaa