Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi dabi ya Kariakoo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jun 2025
Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi dabi ya Kariakoo

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeimarisha ulinzi na usalama kuelekea mechi ya watani wa jadi kati ya Yanga SC na Simba SC itakayopigwa kesho, Jumatano Juni 25, 2025, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo, amewatoa hofu wananchi na mashabiki wa soka kwa kuwataka wajitokeze kwa wingi kushuhudia mchezo huo huku wakizingatia sheria na taratibu. Amewahakikishia usalama wa kutosha kabla, wakati na baada ya mchezo huo muhimu wa Ligi Kuu ya NBC.

Kamanda Murilo ametoa onyo kali kwa watu wenye nia ya kuvuruga amani katika mchezo huo wa dabi maarufu ya Kariakoo, akisema kuwa vyombo vya dola vimejiandaa kikamilifu kuhakikisha wahalifu wanakamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki.

“Hatutavumilia mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vya kihalifu au uchochezi. Tuna vikosi vya kutosha uwanjani na maeneo ya jirani kuhakikisha kila kitu kinaenda salama. Wale wenye nia ya kuleta vurugu, wasithubutu kufika uwanjani,” amesema Kamanda Murilo.

Mchezo huu wa raundi ya pili wa Ligi Kuu, namba 184 ni wa kuamua bingwa wa msimu wa 2024/2025, huku Yanga wakiwa wenyeji wa pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa.

Mara baada ya mechi hiyo, sherehe za kukabidhi kombe kwa bingwa wa ligi zitafanyika uwanjani hapo

Jeshi la Polisi limewataka mashabiki limewataka mashabiki kufuata miongozo ya usalama, na kushirikiana na vyombo vya dola katika kuhakikisha mazingira ya mchezo yanabaki kuwa salama kwa wote.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’