Mechi ya msimu: Yanga SC yapania kutetea heshima na ubingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jun 2025
Mechi ya msimu: Yanga SC yapania kutetea heshima na ubingwa

Leo jioni, macho na masikio ya mashabiki wa soka Tanzania yataelekezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambako Klabu ya Yanga SC itashuka dimbani kuivaa Simba SC katika mchezo wa marudiano wa Dabi ya Kariakoo. Mechi hii ni zaidi ya ushindani wa jadi – ni fainali isiyo rasmi ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/2025, na inaweza kuamua hatma ya taji la ubingwa.

Mchezo huu ulikuwa umepangwa kuchezwa Machi 8, lakini haukufanyika kutokana na sintofahamu ya kiutendaji. Tukio hilo liliacha maumivu kwa wachezaji wa Yanga, ambao walikuwa wamejiandaa kikamilifu na walifika uwanjani kusaka pointi muhimu.

Lakini sasa, mvutano umeisha. Taratibu zimerekebishwa, baadhi ya viongozi wa Bodi ya Ligi wameadhibiwa, na leo mchezo unapigwa rasmi saa 11 jioni. Hakuna visingizio, hakuna kusubiri tena – ni dakika 90 za kuamua nani anastahili kutawala soka la Tanzania.

Nahodha Job: β€œHakuna tunalowaza zaidi ya ushindi”

Katika mkutano na wanahabari uliofanyika jana, nahodha msaidizi wa Yanga, Dickson Job, aliweka bayana msimamo wa timu.

β€œTuko tayari. tumejiandaa vyema, tuna malengo yetu, na tunajua nini kinatakiwa kufanywa, kila dakika itakuwa ya kujitoa kwa hali na mali,” alisema Job kwa msisitizo.

Yanga imekuwa na rekodi nzuri dhidi ya Simba katika mechi nne zilizopita, lakini Job amesisitiza kuwa leo ni mechi mpya, na kikosi kinachoongozwa na kocha Miloud Hamdi kimejipanga kuhakikisha kinamaliza kazi uwanjani, si kwa historia bali kwa vitendo.

Dakika 90 za kuamua hatma

Kwa sasa, Yanga SC inaongoza msimamo wa ligi kwa pointi 79, ikiwa mbele kwa alama moja dhidi ya Simba (78). Hii ina maana kuwa sare pekee leo itawatosha Wananchi kutwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo

Kwa upande wa mashabiki wa Yanga, leo si mechi ya kawaida. Ni fursa ya kuthibitisha uimara wa klabu yao licha ya vizingiti vya nje ya uwanja walivyovikabili msimu huu – vikiwemo maamuzi tata, ratiba tata, na changamoto za kiutawala. Kutwaa taji leo si tu ushindi wa uwanjani, bali ni ushindi wa uvumilivu, mshikamano, na nidhamu ya juu ya kikosi.

Ubingwa wa zaidi ya pointi

Kama Yanga itamaliza mechi ya leo bila kupoteza, itamaliza msimu na pointi 80 au zaidi – idadi sawa au bora kuliko misimu iliyopita. Lakini thamani ya taji la leo ni kubwa kuliko takwimu. Ni taji litakalokuja baada ya msimu wenye mikikimikiki ya kila aina. Ni taji la subira, taji la msimamo, taji la kuamini mfumo wa ndani ya klabu.

Jioni ya leo, Dabi ya Kariakoo itageuka uwanja wa vita wa heshima, historia na hadhi. Kwa Yanga SC, ni mechi ya kuthibitisha ubora na ukubwa wa taasisi hiyo kongwe ambayo ina hisoria ya aina yake tangu enzi za kupigania uhuru

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’