Yanga imeandikisha taji la nne mfululizo ligi kuu ya NBC, baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba
Ni taji la 31 kwa Yanga katika historia lakini ubingwa wa msimu huu ni mtamu zaidi kwa sababu umepatikana mbele ya Simba
Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi na wachezaji wote wanastahili pongezi kwa kazi waliyoifanya leo
Lakini pongezi nyingi kwa uongozi wa Yanga chini ya Rais Injinia Hersi Said na kamati yake ya utendaji, wamehakikisha wanasimamia timu hii ikiwa pamoja na kupigania haki za klabu pale ilipoonekana zinapokwa
GSM na wadhamini wengine wameiwezesha Yanga kiuchumi na kuifanya kuwa na wachezaji bora ambao wanajitoa kuipigania nembo ya timu
Kwa watani huu ni usiku mbaya kwao, lakini wanapaswa kuiheshimu Yanga na kukubali wana safari ndefu kufikia daraja ambalo Yanga ipo
Huu ni ushindi wa tano mfululizo kwa Yanga dhidi ya Simba, wanapaswa kuweka heshima mbele...!


