Baada ya kufanikiwa kutetea kombe la CRDB kwa msimu wa nne mfululizo wakiichapa Singida Black Stars mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa New Amaan Complx hapo jana, kikosi cha Yanga kinarejea leo jijini Dar es salaam wakitokea Zanzibar
Mapokezi ya Yanga yatafanyika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo kikosi kitatua saa 6 mchana
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewaalika mashabiki na wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi Terminl 1 kuipokea timu yao na kufanya paredi la kihistoria
"Tutondoka Zanzibar saa 6:00 mchana na tunatarajiwa kutua JNIA, Terminal 1 saa 6:20 mchana. Hapo tutaanza paredi letu kuelekea Makao Makuu ya Yanga, Jangwani"
"Safari tutaenda kufanya paredi ya aina yake, msimu huu tumevuja jasho jingi sana kutetea makombe haya"
"Paredi letu litakuwa na vituo, pale Msimbazi tutasimama kwa masaa 3 kwani tuna mambo mengi ya kuyatoa moyoni," alitamba Kamwe

Msimu huu umekuwa wa mafanikio makubwa kwa Yanga baada ya kufanikiwa kutetea mataji yote ya ndani huku mwanzoni mwa msimu wakishinda Toyota Cup Afrika Kusini
Yanga imekusanya mataji matano katika msimu huu na pengine hii ni rekodi ya klabu kushinda mataji mengi katika msimu mmojaΒ