Yanga kujipanga Kimataifa zaidi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jul 2025
Yanga kujipanga Kimataifa zaidi

Rais wa Klabu ya Yanga SC, Injinia Hersi Said, amewatoa hofu Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kwa kutoa ahadi ya maboresho makubwa kuelekea msimu ujao wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) 2025/26.

Akizungumza baada ya msimu wa mafanikio kwa Yanga katika soka la ndani, Hersi alikiri kuwa licha ya kutwaa mataji yote ya ndani, timu hiyo haikufanya vyema katika mashindano ya kimataifa msimu uliomalizika. Yanga ilishindwa kuvuka hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika, jambo ambalo amesema limewaacha na masomo muhimu ya kujifunza.

"Tumekuwa na msimu mzuri, tumeshinda mataji matano, lakini tulitereza katika michuano ya Ligi ya Mabingwa," alisema Hersi.

Ameongeza kuwa klabu tayari imeanza kujipanga upya kuhakikisha makosa yaliyopita hayajirudii, huku malengo makuu yakiwa ni kufanya vizuri katika mashindano ya ndani na kimataifa.

"Tunakwenda kujipanga vyema ili kuhakikisha msimu ujao tunafanya vizuri kwenye mashindano ya ndani na kimataifa," alisisitiza kiongozi huyo.

Kauli hiyo ya Hersi inakuja siku moja tu baada ya Yanga kumaliza msimu wa 2024/25 kwa kishindo, kwa kufanya gwaride kubwa la kusherehekea mafanikio yao, lililosimamisha shughuli za jiji la Dar es Salaam kwa takribani saa sita.

Katika msimu huo wa mafanikio, Yanga ilibeba mataji matano: Toyota Cup, Ngao ya Jamii, Muungano Cup, Ligi Kuu Tanzania Bara, na CRDB Bank Cup, mafanikio yaliyoweka historia na kuashiria ubora wa kikosi hicho katika soka la ndani.

Mashabiki wa Yanga sasa wana kila sababu ya kuwa na matumaini, huku macho yao yakielekezwa kwenye usajili, maandalizi ya awali ya msimu, na hatimaye safari ya kuwania taji la Ligi ya Mabingwa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’