Kaimu Kocha wa Yanga Noel Mwandila amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports kesho Jumatano.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa taifa na utaanza saa moja jioni ili kuwapa nafasi mashabiki wengi kuweza kuushuhudia baada ya kumaliza mizunguuko yao ya siku.
Akizungumza na waandishi wa habari leo kuelekea mchezo huo, Mwandila amesema Yanga imeuchukulia mchezo huo kwa umuhimu mkubwa na ndiyo sababu iliamua kutumia kikosi cha vijana kwenye michezo miwili ya ligi ili kuhakikisha kikosi cha kwanza kinafanya maandalizi ya kutosha.
Mwandila amesema Yanga imejipanga kikamilifu na wanaamini wataweza kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
Naye nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema wanatambua uwezo wa Rayon Sports lakini wamefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha wanapata ushindi kesho.
"Tunajua mashindano haya ndiyo nafasi pekee iliyo baki kwetu, tutajitahidi kufanya vizuri.
"Huwezi kumdharau mpinzani,tunafahamu ni timu nzuri ndiyo maana wamefika hapo walipo, tunejiandaa vizuri lengo letu ni kushinda mchezo ili tuweke nafasi nzuri kwenye kundi," amesema.
Nadir amesisitiza umuhimu wa mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kesho kuipa sapoti timu yao kuhakikisha inaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
"Muhimu ni mashabiki kujitokeza kwa wingi ili tushinde pamoja na tuchukue pointi tatu pamoja."

ADVERTISE HERE