Ismaily yajitosa kwa Hamdi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jul 2025
Ismaily yajitosa kwa Hamdi

Taarifa kutoka Misri imebainisha kuwa klabu ya Ismaily inayoshiriki ligi kuu nchini humo iko kwenye mazungumzo kumuajiri Kocha Miloud Hamdi ambaye amemaliza mkataba na Yanga

Kocha huyo aliyeiongoza Yanga kushinda mataji matatu msimu uliomalizika, bado hajasaini mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga licha ya kufanya mazungumzo ya awali na uongozi

Wakati anatua Yanga kuchukua mikoba iliyoachwa na Sead Ramovic, alisaini mkataba wa hadi mwisho wa msimu ambao ulimalizika baada ya mchezo wa fainali kombe la CRDB dhidi ya Singida Black Stars akiiongoza Yanga kushinda mchezo huo kwa mabao 2-0 na kutetea taji la CRDB kwa msimu wa nne mfululizo

Awali Yanga ilianza mchakato wa kusaka kocha ambaye angechukua mikoba baada ya msimu kumalizika lakini kazi nzuri aliyofanya Hamdi katika muda mfupi ni kama imewashawishi mabosi wa Yanga kufikiria kumpa mkataba wa muda mrefu

Hata hivyo bado hakuna taarifa rasmi juu ya hatma yake na upo uwezekano mkubwa anaweza kuibukia Ismaily

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’