Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewakumbusha Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kulipa ada zao ili waiwezeshe klabu kiuchumi
Mwaka Mpya wa fedha umeanza Julai 01 hivyo kila Mwanachama au Shabiki ambaye amesajiliwa ana jukumu la kulipa ada yake huku wale ambao hawajasajiliwa wakitakiwa kujisajili katika Matawi
Kamwe amesema kuna gharama kubwa ya kuwa na timu bora ya kutwaa mataji mfululizo hivyo kila Mwanayanga anapaswa kuwajibika ili kuhakikisha mataji yanaendelea kumiminika Jangwani
"Hii Yanga ni klabu ya Wanachama hivyo ni jukumu la kila Mwanachama kutimiza wajibu bila hivyo tunaweza kurudi kule tulikotokea jambo ambalo hatupendi lijirudie"
"Wakati huu kuna wachezaji wengi muhimu wamemaliza mikataba na tunapaswa kuwapa mikataba mipya haraka. Lazima tuambiane ukweli timu inahitaji fedha na sisi wanachama ni lazima tufahamu hili ni jukumu letu," alisema Kamwe
Yanga imesajili karibu Wanachama laki moja lakini changamoto ipo katika ulipaji wa ada kwa wakati