Mokwena? mbona inawezekana kwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jul 2025
Mokwena? mbona inawezekana kwa Yanga

Baada ya Kocha Miloud Hamdi kuondoka akijiunga na Ismailia kama Mkuguenzi wa ufundi wa klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Misri, jina la kocha mahiri kutoka Afrika Kusini, Rulani Mokwena limerejea tena katika viunga vya Jangwani

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, zimethibitisha kuwa Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said alifanya mazungumzo na Mokwena ambaye kwa sasa bado hana timu baada ya kuachana na Wydad

Yanga ikiwa na malengo makubwa ya kufanya vyema katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao, inahitaji kocha aina ya Mokwena ambaye ana uzoefu mkubwa wa kucheza hatua za robo fainali, nusu fainali na hata fainali wakati akiwa na Mamelodi

Ingawa muda wake na Wydad ulikuwa mfupi, aliisaidia klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye ligi ya Morocco na kufuzu CAF Confederation Cup (CAF CC), hatua ambayo inachukuliwa kama mafanikio ukizingatia hali ya awali ya klabu hiyo kabla ya kuwasili kwake.

Kuja kwa kocha kama Mokwena ambaye ana rekodi inayovutia hasa wakati yuko Mamelodi, kunaweza kuwa hatua madhubuti ya kuimarisha kikosi kuelekea kufanikisha malengo ya klabu

Wapo wenye wasiwasi kama Yanga itaweza kumlipa Mokwena? lakini wakati mwingine makocha hawaangalii maslahi pekee, bali pia miundombinu na mfumo wa kiutendaji ndani ya klabu.

Katika moja ya mahojiano yake, Mokwena alifichua kuwa Wydad hawakumlipa mshahara kwa miezi kadhaa na mpaka sasa anawadai. Kuna wakati alilazimika kuwalipa baadhi ya watu wake katika benchi la ufundi kutokana na ukata ulioikumba Wydad

Yanga ina uchumi wa wastani pia ikiwa miongoni mwa klabu chache zinazoendeshwa kisasa barani Afrika. Sasa ina uwezo wa kusajili wachezaji bora na mazingira yake yanaweza kumshawishi kocha yeyote kujiunga nayo

Mokwena anaweza kuwa alama mpya ya mabadiliko makubwa, hasa katika kuhakikisha timu inavuka hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na kupata mafanikio makubwa zaidi kuliko miaka ya nyuma.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’