Karia atangazwa kuwa mgombea pekee wa Urais TFF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jul 2025
Karia atangazwa kuwa mgombea pekee wa Urais TFF

Kamati ya Uchaguzi ya TFF Imewang'oa wagombea watano wa nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kubaki na jina moja la Wallace Karia anayetetea kiti hicho.

Akitangaza ripoti ya usahili wa uchaguzi huo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF Wakili Kiomoni Kibamba, amesema Karia ndiye mgombea pekee aliyekidhi vigezo na kwa mujibu wa Kanuni na kama kuna mtu anapingamizi bado ana nafasi ya kufanya hivyo

"Waliotia nia kugombea nafasi ya usais wa TFF walikuwa sita, mmoja hakuja kwenye usaili wakabaki watano, wanne wana mgogoro na kanuni na mgombea mmoja (Wallace Karia) yeye amekidhi vigezo vyote kwa hiyo yeye hakuwa na mgogoro na kanuni"

"Kwa upande wa waliotia nia kugombea ya ujumbe waliohudhuria zoezi la usaili ni watia nia 17, watia nia 10 wamekidhi vigezo vya awali vya kuingia kwenye uchaguzi wakisubiri mchato wa mapingizi"

"Wagombea saba waliobaki walikuwa na mgogoro na kanuni, maana yake hawakukidhi vigezo na masharti. Kama mtu hakuridhika na maamuzi ya kamati ya Uchaguzi ana haki ya kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ambayo ikifanya maamuzi inatuletea sisi ili tuendelee na mchakato,"alisema Kibamba

Hata hivyo hatma ya mchakato huo inasubiri kile kitakachoamuliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kufuatia jopo la Mawakili watano kumuweka pingamizi Rais Karia kugombea tena nafasi hiyo kwa awamu ya tatu pia wakipinga kujimilikisha endorsement zote kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’