Yanga imeshindwa kuibuka na ushindi nyumbani kwenye mchezo wa pili kombe la Shirikisho kundi D baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Rayon Sports.
Yanga iliuanza mchezo huo kwa nguvu na kufanikiwa kupata kona kwenye dakika ya kwanza ya mchezo, kona ambayo hata hivyo haikuzaa matunda.

Licha ya kufanya mashambulizi kadhaa kwenye kipindi cha kwanza, Yanga ilikosa mbinu ya kuipenya ngome ya Rayon hivyo kupelekea kupiga mipira bila mpangilio.
Kwenye kipindi cha pili ni Rayon Sports iliyokuwa hatari zaidi kwa kupeleka mashambulizi langoni kwa Yanga.

Lakini kukosa umakini kwa washambuliaji wake pamoja na uimara wa kipa Rostand kuliinusuru Yanga isifungwe.
Yanga ilipoteza nafasi pekee kwenye dakika ya 68 baada ya mpira wa Obrey Chirwa aliopiga hatua chache kutoka langoni kwa Rayon kugonga mwamba.

Thabani Kamusoko ambaye alionekana kucheza vizuri leo alipumzishwa kwenye dakika ya 65 na nafasi yake kuchukuliwa na Raphael Daudi, mabadiliko ambayo hayakuwafurahisha mashabiki wengi waliofika uwanja wa Taifa kuushuhudia mchezo huo.

Matokeo hayo yanaibakisha Yanga mkiani mwa kundi D ikiwa na alama moja.
Aidha nayo Gor Mahia imelazimishwa suluhu ya bila kufungana na USM Alger katika mchezo uliopigwa nchini Kenya.
USM ALger inaongoza kundi D ikiwa na alama nne wakati Gor Mahia na Rayon Sports zina alama mbili kila moja.
Matokeo ya sare huko Kenya yanaipa Yanga ahueni lakini italazimika kupata matokeo itakapoenda Kenya na Rwanda ili kuwa na nafasi ya kutinga robo fainali

ADVERTISE HERE