Klabu ya Yanga inatajwa kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Tabora United, Offen Chikola, imefahamika
Chikola anatarajiwa kutua Yanga akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba kunako klabu ya Tabora United
Msimu uliopita ulikuwa bora sana kwa Chikola akipachika mabao 8 na kuwa kinara wa mabao katika kikosi cha Tabora United
Usajili wa Chikola ni sehemu ya mkakati wa Yanga kuongeza ushindani katika safu ya kiungo cha ushambuliaji, akiwa na uwezo wa kutumika kama winga au namba 10
Aidha nyota huyo anatarajiwa kuchukua nafasi ya Farid Mussa aliyemaliza mkataba na Yanga. Klabu ya Mbeya City inapambana kumsajili Farid ambaye alikosa sehemu kubwa ya msimu uliopita akiwa majeruhi
ADVERTISE HERE