Mwenyekiti wa umoja vilabu barani Afrika (ACA) Injinia Hersi Said amethibitisha Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kuidhinisha ongezeko la fdha za maandalizi kwa ajili ya klabu zinazoshiriki ligi ya mabingwa n kombe la Shirikisho msimu ujao
Msimu uliopit klabu zilipewa dola 50,000 lakini msimu zitapewa dola 100,000 zaidi ya Tsh Milioni 260
Ikumbukwe baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa ACA mwaka jana, jukumu la kwanza alilofanya Hersi ni kuomba fedha hizo za maandalizi kwa klabu ambazo awali hazikuwa zikitolewa
Na sasa amefanikisha ongezeko hilo ambalo litanufaisha klabu zote zitakazoshiriki CAF CL na CAF CC
"Nina furaha kubwa kushiriki habari za mageuzi kutoka Rabat, ambako ninahudhuria mkutano wa Kamati Tendaji ya CAF (EXCO)."
"Baada ya majadiliano ya kujenga kati ya Chama cha Vilabu vya Afrika (ACA) na Rais wa CAF Dkt. Patrice Motsepe, CAF imeamua rasmi kuongeza fungu la msaada kwa vilabu vinavyoondolewa katika raundi za awali kutoka dola 50,000 hadi dola 100,000 kuanzia msimu wa 2025/26"
"Mabadiliko haya makubwa yanaonyesha dhamira ya CAF ya kuimarisha soka la vilabu barani Afrika na kuhakikisha kuwa vilabu zaidi vinapata rasilimali za kukua na kushindana katika ngazi za juu zaidi. Shukrani za dhati kwa uongozi wa CAF chini ya Rais Dkt. Motsepe," aliandika Hersi katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii