Doumbia afurahia kutua Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jul 2025
Doumbia afurahia kutua Yanga

Kiungo fundi kutoka Ivory Coast, Mohammed Doumbia, ameonyesha furaha yake baada ya kukamilisha usajili wake kujiunga na mabingwa wa kihistoria nchini Tanzania, Yanga SC.

Doumbia, mwenye umri wa miaka 26, anatajwa kuwa mmoja wa usajili wa mapema zaidi kufanywa na klabu hiyo katika dirisha hili la usajili.

Doumbia aliwasili nchini mapema mwezi Juni na alifanya mazoezi na kikosi cha Yanga pale Avic Town, Yanga ikionyesha dhamira ya kumuweka kwenye mipango yao ya msimu mpya.

Akiwa bado hajaanza kuichezea timu rasmi, aliungana na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, na wachezaji wengine waliokuwa nje ya kikosi kilichoshuka dimbani dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa visiwani Zanzibar.

Akizungumza na chombo cha habari nchini kwao, Ivory Coast, Doumbia alisema:
"Najivunia kujiunga na timu kubwa kama Yanga. Lengo langu ni kutwaa makombe na kufanya historia Tanzania."

Doumbia ni kiungo anayeweza kucheza nafasi zote eneo la kati yaani namba 6, 8 na hata 10, akiwa mahiri katika kupiga pasi, ana kasi, nguvu na umahiri wa aina yake anapokuwa na mpira mguuni. Anawasili kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na FC Majestic ya Burkina Faso. Mbali na hapo, amewahi pia kuitumikia klabu ya Slovan Liberec ya Jamhuri ya Czech.

Usajili wake unaonekana kuwa sehemu ya mikakati ya Yanga kujijenga zaidi kuelekea msimu mpya, hasa kwa kuimarisha safu ya kiungo yenye ubunifu na uwezo wa kushambulia.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’