Yanga yapokea Milioni 262 kutoka SportPesa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jul 2025
Yanga yapokea Milioni 262 kutoka SportPesa

Kampuni ya SportPesa imeipongeza klabu ya Yanga kwa kufanikiwa kutwaa mataji yote ya ndani msimu uliopita

SportPesa leo wametoa bonasi kwa Yanga kufuatia mafanikio waliyopata msimu uliomalizika kwa kushinda mataji matano

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kampuni ya SportPesa, Abbas Tarimba amesema msimu uliomalizika ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Yanga na wanawapongeza kwa mafanikio hayo

Kutokana na makubaliano ya kimkataba, Tarimba amesema SportPesa imetoa bonasi ya Tsh Milioni 262 kwa Yanga

"Sisi kama SportPesa, wadhamini wakuu wa Yanga, katika kipindi cha miaka 8 iliyopita tumetimiza vyema majukumu ya kimkataba"

"Hivyo leo nichukue nafasi hii kutangaza kuipa Yanga Tsh Milioni 262 kama bonasi kutokana na mafanikio ya msimu uliopita"

"Sportpesa tunawapongeza sana Viongozi wa Yanga kwa namna ambavyo wameibadilisha hii Klabu. Yanga imepata mafanikio kwenye msimu ambao ulikuwa mgumu sana. Kubeba mataji matano sio jambo dogo kabisa katika historia ya nchi hii. Huu ndio mwaka bora kabisa katika historia ya Klabu hii"

"Tunawataka muendelee mafanikio haya msimu ujao na zaidi mhakikishe mnaleta kombe la Afrika (CAF CL) ambao mlilikosa msimu uliopita," alisema Tarimba

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema wanaishukuru kampuni ya SportPesa kwa kuidhamini Yanga kwa kipindi cha miaka 8

"Katika kipindi cha miaka nane ya udhamini wa SportPesa tumeshinda mataji mengi. Mafanikio haya ni taswira ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya SportPesa na Yanga"

"Kwa kuzingatia makubaliano ya kimkataba, tunafahamu tuko katika majadiliano kwa ajili ya kuhuisha mkataba, nikuhakikishie Mwenyekiti, hatutakuwa na sababu ya kwenda kwa Mdhamini mwingine"

"Niwapongeze SportPesa hatujawahi kuwa na malalamiko ya malipo kutoka SportPesa, wametimiza wajibu wao wa kimkataba"

"Nikuhakikishie tutakwenda kuhakikisha mahusiano yanadumu na yanakwenda mbele zaidi, tutatimiza vyema jukumu letu la kuipa thamani SportPesa," alisema Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’