Yanga kufanya usajili wa kimkakati kwa ajili ya CAFCL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jul 2025
Yanga kufanya usajili wa kimkakati kwa ajili ya CAFCL

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema anajua shauku ya Wanachama na Mashabiki wa Yanga ni kuona timu hiyo inafanya vyema zaidi na kufika mbali katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF CL)

Akizungumza katika hafla ya kupokea bonasi ya Tsh Milioni 262 kutoka kwa wadhamini SportPesa baada ya msimu wa mafanikio, Hersi amesema Yanga ina deni katika michuano ya Kimataifa kwa kuwa hawakufanya vizuri sana msimu uliopita

Amesema kupitia dirisha hili la usajili, watafanya usajili wa kimkakati ili kuhakikisha wanasajili wachezaji bora ambao wataisaidia Yanga kufanya vyema katika michuano hiyo msimu huu

Hersi amesema malengo ya chini ya Yanga ni kufika hatua ya makundi ambapo kama watafanikiwa wataweka malengo mapya kuanzia hatua hiyo

"Baada ya mafanikio tuliyopata msimu uliomalizika, najua msimu ujao kutakuwa na ugumu zaidi kwahiyo Wanachama na wapenzi wa klabu ya Yanga muendelee kutuunga mkono na tutahakikisha tunapambania makombe yetu"

"Na lile ambalo linazungumzwa na mashindano ya Kimataifa deni kubwa tunalo msimu ujao 2025/2025 nafikiri focus yetu kubwa itaelekezwa huko na focus hii itaanza kwenye maandalizi mazuri lakini tutafanya usajili bora ambao tutafanya kwenye msimu huu"

"Kiukwel hatujawa na matokeo mazuri kwenye michuano ya Kimataifa ya mfululizo kama tuliokuwa nayo hapa ndani na mashindano ya Afrika ni mashindano ambayo yanahitaji maandalizi makubwa"

"CAFCC tulifika fainali, baadae tukafika robo fainali CAF Champions League kwa sababu tulikuwa hatujaingia kwa miaka 25 na baadae msimu huu tukaishia makundi Kwahiyo kwa msimu ujao malengo ya Yanga ni kuingia kwenye makundi na tukishaingia kwenye makundi tutabadilisha upepo"

"Tukishaingia kwa msimu wa tatu mfululizo tunatengeneza malengo mapya, tutafanya usajili ambao ni wa kimalengo na kimkakati na wachezaji watakaokuja kwa sababu watakuwa ni wenye ubora nao hawataishia makundi," alisema Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’