Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema michakato ya maboresho ya kikosi imekamilika kwa asilimia 85
Kamwe amesema michakato iliyobaki inaendelea kukamilishwa kabla ya timu kurejea tayari kwa maandalizi ya msimu mpya
"Tumeshakamilisha asilimia 85 ya timu tunayoijenga kwa ajili ya msimu ujao bado asilimia 15 ili tukamilishe michakato yote"
"Baada ya hapo wiki ya mwisho ya mwezi wa saba timu inatakiwa ianze kuripoti kwa ajili ya vipimo na utambulisho wa kocha kabla ya kuanza maandalizi ya msimu ujao mwanzoni mwa August," alisema Kamwe
Aidha katika michakato hiyo ya usajili, Kamwe amefichua Yanga kusajili mchezaji aliyekuwa katika mazungumzo na moja ya timu kubwa hapa nchini
"Wako wachezaji tuliwakuta baadhi ya timu zinazungumza nao, lakini kwa sababu hizo timu maamuzi yao yanafanywa na watu wasiopungua hamsini, sisi tumepita nao"
"Yuko mchezaji mmoja alituambia mimi nina mkataba na moja ya timu hapo Tanzania, lakini nasubiri wanipe uthibitisho na kuna fedha bado hawajanitumia, watu wakaangalia na tukaona huyu anatufaa nae tukapita nae, " alitamba Kamwe
Akizungumza kuhusu mchakato wa kumpata kocha mpya Kamwe amesema tayari kocha amepatikana kinachosubiriwa ni kumtambulisha
Amesema uteuzi wa kocha huyo umezingatia mipango ya Yanga ya msimu ujao, ni kocha mwenye kiu ya mafanikio kama ilivyo Yanga