Kiungo Clatous Chama raia wa Zambia, yuko mbioni kujiunga na klabu ya Azam Fc, imefahamika
Chama alikuwa katika mazungumzo ya kuongeza mkataba na Yanga lakini inaelezwa mazungumzo hayo hayakupata mwafaka
Mkataba wake umemalizika, ni mchezaji huru, taarifa ya duru za usajili imethibitisha Chama kufanya mazungumzo na Azam Fc ambayo yamefikia mwafaka na nyota huyo huenda akaelekea Chamazi
Katika dirisha hili la usajili Yanga imepania kufanya maboresho makubwa kwa kusajili wachezaji wenye sifa ya kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza ili kuwapa changamoto wachezaji waliopo
Msimu wake mmoja alioitumikia Yanga Chama amefunga mabao sita na kutoa pasi nne za mabao (ligi kuu)
ADVERTISE HERE