Ikangalombo asikilizia hatma yake Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jul 2025
Ikangalombo asikilizia hatma yake Yanga

Winga Mcongoman Jonathan Ikangalombo anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao Yanga imepanga kuwatoa kwa mkopo katika dirisha hili la usajili lililofunguliwa tangu Julai 1 na likitarajiwa kufungwa Septemba 07

Akiwa ameitumikia Yanga kwa takribani miezi sita tu, Ikangalombo ameshindwa kupenya katika kikosi cha kwanza

Wakati anasajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria, Ikangalombo alisaini mkataba wa miaka miwili na nusu hivyo bado ana mkataba wa miaka miwili

Inaelezwa wawakilishi wa mchezaji huyo wamegomea mpango wa Yanga kumtoa kwa mkopo wakishinika mkataba wake uvunjwe ili akatafute changamoto mpya katika timu nyingine

Mpaka wakati nyota huyo anaondoka nchini kurejea kwao DR Congo kwa ajili ya mapumziko, hakukuwa na mazungumzo yoyote baina yake na Yanga kuhusu hatma yake

Ni wazi katika kipindi cha wiki mbili kabla ya wachezaji kuanza kurejea tayari kuanza pre-season, hatma yake itakuwa imefahamika

Tangu atuje Yanga, Ikangalombo amecheza mechi sita za Ligi Kuu akitumia dakika 136 akiasisti mara mbili, bila kufunga bao

Katika Kombe la Shirikisho (FA) alifunga bao moja katika hatua ya 16 Bora katika mchezo dhidi ya Songea United Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’