Mlinzi wa kushoto wa Yanga Nickson Kibabage yuko katika mazungumzo na uongozi wa Singida Black Stars ili kujiunga na timu hiyo, imefahamika
Kibabage bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Yanga lakini upo uwezekano atatua Singida BS kwa mkopo wa msimu mzima
Yanga na Singida BS pia zinafanya mazungumzo kuhusu hatma ya Israel Mwenda ambaye muda wake wa mkopo wa miezi sita umemalizika

Yanga inataka kumsajili Mwenda moja kwa moja baada ya kuridhishwa na uwezo wake
Jana Singida BS ilitangaza kumsajili Kelvin Kijili aliyekuwa akiitumikia Simba, usajili huo ni dalili kwa Yanga kufanikiwa kumbakisha Mwenda
ADVERTISE HERE