Klabu ya Yanga inatajwa kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji wa CS Sfaxien Moussa Balla Conte raia wa Burkina Faso kwa mkataba wa miaka miwili
Taarifa kutoka ndani ya uongozi imebainisha kuwa Yanga ilikamilisha usajili wa kiungo huyo Ijumaa usiku baada ya kufanikisha malipo ya dau la usajili kwa Sfaxien
Yanga iliingilia mchakato wa kumsajili kiungo huyo siku chache zilizopita, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe akidokeza 'umafia' waliowafanyia watani zao Simba ambao walikuwa katika hatua za mwisho kumsajili
Hata hivyo inaelezwa haikuwa rahisi kwa Yanga kukamilisha usajili huo baada ya Simba kurejea na dau kubwa kabla ya GSM kufunga hesabu kwa kulipa dau lote kwa mkupuo mmoja wakati Simba waliomba kulipa fedha hizo kwa awamu mbili
Inaelezwa mchezaji huyo ameidhinishwa na Kocha Mpya wa Yanga baada ya tathmini aliyofanya ya kikosi
Conte antarajiwa kuchukua nafasi ya Clatous Chama aliyemaliza mkataba