Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine
Wakati Senzo Mbartha anaondoka, Wananchi walikuwa na hofu kuwa msingi uliokuwa umeweka na raia huyo wa Afrika Kusini, unaweza kuyumba baada ya kuondoka kwake
Lakini ujio wa Mtine sio tu umeendeleza pale alipoishia Mbartha, bali umeleta mengi mazuri, Yanga ikifurahia mafanikio hasa katika michuano ya CAF
Katika kipindi chake, Yanga imecheza fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC), imecheza robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa (CAF CL) na hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa
Yanga imeendelea kutetea mataji ya ligi kuu, kombe la FA na Ngao ya Jamii
Utuivu unaoonekana katika utendaji wa shughuli za klabu ya Yanga ni kutokana na uongozi thabiti wa Mtine akiwa ndiye msimamizi mkuu
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake..
