Kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki ameripoti rasmi katika kambi ya Wydad Athletic kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa mashindano 2025/26
Kuripoti kwake kambini kunamaliza uvumi uliokuwa mitandaoni juu ya hatma ya kiungo huyo aliyejijengea heshima kubwa akiwa na klabu ya Yanga
Wydad walikamilisha usaili wa Aziz Ki Julai 10 ikiwa ni awamu ya pili ya makubaliano yao na Yanga

Wakati Aziz Ki anajiunga na Wydad mwanzoni mwa Juni kushiriki michuano ya kombe la Dunia la klabu, walilipa sehemu ya dau walilokubaliana na Yanga lakini walipewa muda maalum wa kukamilisha mchakato huo ifikapo Julai 10
Aziz Ki amejiunga na Wydad kwa mkataba wa miaka miwili akiingizia Yanga kiasi cha Tsh Bilioni 1.7
ADVERTISE HERE