Kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga Celestin Ecua ni kama ameona utambulisho wake rasmi Yanga unachelewa hivyo kuamua kujitambulisha mwenyewe
Kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Instagram ambao umethibitishwa, Ecua amejitambulisha kama mchezaji wa zamani wa Zoman Fc anayetua Yanga
Mshambuliaji huyo aliyekuwa anakipiga ASEC Mimosas kwa mkopo akitokea Zoman FC, tayari amekamilisha taratibu zote za usajili wake na Yanga
Ecua mwenye miaka 23, ana kasi, chenga na jicho la kuliona lango. Anatarajiwa kuongeza ushindani kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga akimudu vyema kucheza nafasi zote za mbele katika eneo la ushambuliaji.
Akiwa Ivory Coast msimu uliopita, alifunga mabao 15 na kutoa asisti 12 kwenye Ligi Kuu. Kimataifa amecheza jumla ya mechi tano na kufunga mabao mawili. Anatarajiwa kuwasili nchini mwishoni mwa wiki kuweka sawa mipango ya maisha yake hapa Tanzania
Kama mchezaji mpya wa kigeni Yanga inapaswa kukamilisha taratibu za vibali vyake pamoja na makazi ili kuhakikisha anakuwa tayari kuungana na wenzake pale pre-season itakapoanza
Nyota mwingine mpya aliyesajiliwa na Yanga Mohamed Doumbia tayari yuko nchini akiendelea na mazoezi binafsi kujiweka fit kabla ya pre-season kuanza