Yanga yajipanga kusaka vipaji michuano ya CHAN 2024

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jul 2025
Yanga yajipanga kusaka vipaji michuano ya CHAN 2024

Yanga inatarajiwa kutumia michuano ya CHAN 2024 itakayoanza August 02 hadi August 30 kusaka wachezaji mahiri wa kuwasajili, imefahamika

Akizungumza hivi karibuni, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisema usajili wa timu hiyo umekamilika kwa asilimia 85

Kigogo mmoja wa Yanga amenukuliwa na Mwanaspoti,  akibainisha kuwa wataacha nafasi chache ili kuangalia wachezaji wengine kwenye michuano ya CHAN akieleza shida kubwa ni kupata mastaa wenye ubora lakini suala la fedha si tatizo kwao.

Kwa mujibu wa bosi huyo, walichopanga ni kwa baadhi ya nafasi wanazotaka kuziboresha kwenye kikosi chao watakuwa na mkakati maalum wa kuangalia watu bora watakaopatikana kwenye fainali hizo.

Bosi huyo wa juu Yanga anayehusika kwenye usajili, alisema wachezaji wote wanaoshiriki fainali hizo, ni wale wanaocheza ligi za ndani Afrika, hivyo wanaona hakutakuwa na ugumu mkubwa kwao kuwapata.

“Hatuwezi kumaliza nafasi zote, tutakuwa na jicho letu kwenye hizi Fainali za CHAN, unajua shida yetu sisi ni watu bora tunaowataka, sio fedha"

“Kama ingekuwa fedha tusingeingia sehemu ambazo kuna timu unaambiwa inazunguka na mchezaji ikiongea naye, tunataka watu sahihi kwa malengo yetu"

“Kuna wachezaji tutawatafuta kwenye fainali hizi, tumejipanga kwenda Uganda, Kenya na hapa nchini kufuatilia kwa kina wachezaji bora tunaowataka,” alisema

Michuano hiyo inafanyika katika kipindi ambacho dirisha la usajili liko wazi kwani litafungwa Septemba 7 huku michuano hiyo ikitarajiwa kufika tamati August 30

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’