Yanga ni kama imeachana na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Singida Black Stars Jonathan Sowah raia wa Ghana sasa ikihusishwa na Andy Boyeli raia wa DR Congo
Boyeli anaitumikia klabu ya Sekhukhune inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini
Inaelezwa Kocha Mpya wa Yanga Romain Folz ndiye aliyependekeza usajili wa mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita alifunga mabao sita katika mechi 27 ligi kuu ya Afrika Kusini
Msimu wa 2022/23 Boyeli aliitumikia Power Dynamos ya Zambia ambapo alitwaa kiatu cha mfungaji bora baada ya kufunga mabao 18 huku akitwaa tuzo ya MVP
Kulingana na Lorenz Kohler, mwanahabari maarufu wa Afrika Kusini, Yanga itamsajili Boyeli(24) kwa mkopo wa mwaka mmoja huku kukiwa na kipengele cha kumsajili moja kwa moja kama itaridhishwa nae
Boyeli atatua Yanga kuchukua nafasi ya Kennedy Musonda aliyetimkia Urusi baada ya mkataba wake kumalizika