Kiungo mahiri Mudathir Yahya bado yupo sana na Wananchi kwani mabingwa hao wa soka Tanzania Bara wamethibitisha ameongeza mkataba
Ukizungumzia wachezaji waliokuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Yanga kwenye misimu miwili iliyopita, Mudathir ni mmoja wao
Kulikuwa na majaribio ya hapa na pale kumn'goa Mudathir lakini mwenyewe amechagua kuendelea kufurahi na Wananchi
Yanga iliweka wazi malengo yake baada ya msimu kumalizika; kuwaongezea mikataba wachezaji wote waliomaliza mikataba ambao wamependekezwa kuendelea kuwa sehemu ya kikosi
Lakini pia kusajili wachezaji bora ambao wataifanya Yanga iendelee kuishi katika malengo yake ya kushinda mataji
ADVERTISE HERE