Kamwe amtaja Hersi usajili wa Conte

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jul 2025
Kamwe amtaja Hersi usajili wa Conte

Katika dirisha hili la usajili, Klabu ya Yanga imefanikiwa kufanya moja ya usajili mkubwa kwa kumtambulisha rasmi kiungo mkabaji Moussa Balla Conte, raia wa Guinea aliyetua kutoka klabu ya C Sfaxien.

Lakini nyuma ya pazia la mafanikio haya, ipo hadithi ya ushawishi mkubwa wa Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said, ambaye anatajwa kuwa silaha ya ushindi kwenye dili hilo lililokuwa na ushindani mkali.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, amefichua siri nzito za namna Hersi alivyosimamia na kuiongoza mikakati ya kumnasa Conte, licha ya mchezaji huyo kuwindwa na timu kadhaa, ikiwemo watani wao wa jadi Simba SC.

Mazungumzo ya Ana kwa Ana Yaliyovunja Mipango ya Simba

Kamwe amesema hatua ya Hersi kuzungumza ana kwa ana na Conte ilibadilisha kila kitu. Katika mazungumzo hayo, Conte alihamasishwa kwa nguvu zaidi kuhusu maono ya Yanga, nafasi yake katika kikosi, na mipango ya maendeleo ya klabu hiyo. Ushawishi wa Hersi, kwa mujibu wa Kamwe, ndiyo uliokuwa silaha ya kwanza iliyoleta ushindi.

"Wakati tetesi zikiendelea mitandaoni, sisi tulikuwa tumeshamsajili Conte tangu Julai 11, baada ya mzungumzo kati yake na Rais wetu Injinia Hersi Said," alisema Kamwe.

Mapendekezo ya Kocha, Uwekezaji wa GSM na Hatua za Haraka

Kamwe ameeleza kuwa usajili wa Conte ulikuwa maombi maalum ya kocha mkuu mpya wa Yanga, ambaye alihitaji kiungo mkabaji mahiri mwenye uwezo mkubwa wa kuzuia. Baada ya tathmini ya kikosi, Conte akateuliwa kama chaguo sahihi zaidi.

Baada ya kupokea mapendekezo ya kocha, Hersi alifanya mawasiliano ya haraka na wakala wa mchezaji na klabu ya CS Sfaxien, kuhakikisha taratibu zote zinaenda kwa kasi. Katika hatua hizo, mchango wa mwekezaji GSM ulihitajika kukamilisha dili hilo kifedha.

"Silaha ya pili tuliyotumia ni nguvu ya uwekezaji kupitia GSM waliogharamia kila kitu mara baada ya kufikia makubaliano," Kamwe alibainisha.

Simba Walijaribu Lakini…

Kamwe pia ameweka wazi kwamba Simba walijaribu kwa nguvu zote kumpata Conte, wakimtumia kocha wao pamoja na kipa Camara ambaye ni rafiki wa mchezaji huyo, lakini Conte alishawishika zaidi na mradi wa maendeleo ya Yanga.

ITC na Utambulisho wa Haraka

Mchakato ulifungwa rasmi Ijumaa usiku Conte aliposaini mkataba, kabla ya chama cha soka Tunisia (FTF) kutuma ITC Jumamosi iliyofuata. Kutokana na presha kubwa kutoka kwa timu nyingine zilizokuwa zikiendelea kumfuata Conte, Yanga ililazimika kumtambulisha mchezaji mapema zaidi ya ilivyopangwa.

"Yeye mwenyewe alituomba tumtambulishe mapema ili kuondoa presha. Hata akiwa hapa nchini kukamilisha taratibu, bado simu za ofa zilikuwa zinaendelea kumiminika," Kamwe alimalizia.

Conte ametua Yanga kuimarisha safu ya kiungo cha ukabaji baada ya tathmini ya kocha mpya kutoa majibu kuwa viungo waliopo ni bora katika sifa walizonazo lakini sio viungo wakabaji asili.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’