Rais wa Yanga Injinia Hersi Said aliweka ahadi kuwa usajili atakaofanya katika dirisha hili utakuwa bora pengine kuliko wakati mwingine wowote tangu alipokabidhiwa majukumu ya kuiongoza Yanga
Hersi ameishi katika maneno yake baada ya Yanga kutambulisha usajili wa pili katika dirisha hili, Offen Chikola aliyetua kutoka klabu ya Tabora United
Ukitaja majina ya wachezaji watano wa ndani waliong'ara katika ligi kuu ya NBC msimu uliopita, Chikola hatakosekana
Kiungo mshambuliaji mahiri anayetumia mguu wa kushoto, amepata nafasi ya kuwaonyesha Wananchi ubora wake
Wakati yuko Tabora United, Chikola ndiye aliyekuwa 'star' wao akimaliza msimu na mabao nane
Pengine hakuzungumzwa sana kwa kuwa alikuwa akicheza timu ndogo lakini kwa kuwa ametua Yanga, mashabiki wa soka watatambua thamani yake
