Kouma ametimiza ndoto kutua Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jul 2025
Kouma ametimiza ndoto kutua Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Lassine Kouma amefichua kuwa alikuwa na ndoto ya kuichezea Yanga siku moja, kusajiliwa na mabingwa hao wa nchi ni kama ndoto yake imekamilika

Juzi Yanga ilitangaza kumsajili Co-Magic akitua kutoka klabu ya Stade Malien ya huko Mali

Kouma amesema aliifahamu Yanga tangu mlinda lango Djigui Diarra alipojiunga nayo na misimu miwili iliyopita Yanga walipokwenda Mali kucheza dhidi ya Real Bamako alipata nafasi ya kuwaona uwanjani na kumfanya atamani zaidi kujiunga na mabingwa hao wa nchi

"Nimeifuatilia Yanga tangu Djigui Diarra alipofika hapa, pia niliwafuatilia walipokuja Mali kucheza na Real Bamako"

"Niliona namna Djigui alivyokuwa na furaha sana lakini pia jinsi timu ilivyokuwa imejipanga hivyo tangu wakati huo nilikuwa na shauku kubwa ya kucheza hapa siku moja maana nilikuwa kama shabiki toka nilivyowajua" alisema Kouma

Kouma amebainisha kuwa baada ya kupewa taarifa kuwa Yanga inataka kumsajili, alipokea wito huo kwa furaha kubwa

Pia kiungo huyo fundi ameeleza kuwa Diarra amemjulisha mambo mengi kuhusu klabu ya Yanga ikiwa ni pamoja na kufahamu ukubwa wa klabu hii

"Djigui aliniambia Yanga ni timu nzuri na klabu kubwa sana, pia alinieleza mambo mengi lakini alinisisitizia kuwa nimejiunga na timu kubwa sana"

Kouma ana historia ya kipekee katika klabu ya Stade Malien kwani alijiunga na timu hiyo akiwa na miaka 10 katika akademi yao ambapo amecheza katika madaraja yote ya ukuaji kama mchezaji kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa msimu wa 2022/23

Kouma amefichua katika muda wote ambao ameitumikia Stade Malien alikuwa mchezaji kipenzi wa viongozi na mashabiki wa klabu hiyo

Amewaomba Wanayanga wampokee kama mtoto wao huku akiahidi kufanya mambo makubwa ya kuwafurahisha pengine zaidi ya huko alikotoka

"Ningependa kuomba na kuwasihi mashabiki wa Yanga , viongozi, benchi la ufundi na kila mmoja ndani ya klabu mnipe nafasi hiyo ya kuwa kama mtoto wenu hapa Tanzania"

"Nitajitahidi kwa kiwango changu na kujitoa kwa moyo wangu wote na kufanya kazi kwa bidii ili niweze kukamilisha nafasi niliyopewa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
1h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
4h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’