Wiki iliyopita Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alikuwa Kibaha kushiriki mechi maalum ya hisani ambayo iliandaliwa na mlinda lango Aboubakar Khomein
Baada ya mechi hiyo wananchi wa Kibaha wakamuomba Injinia Hersi aondoke na mchezaji Juma Popo wakiamini ni kijana mwenye kipaji kikubwa
Hersi aliridhia ombi la Wananchi na kuondoka na kijana huyo na akamjumuisha katika kikosi cha Yanga kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wa Safari Lager Cup dhidi ya Safari Lager talents
Hatimaye juzi Popo akapata nafasi ya kuichezea Yanga ambapo alipewa dakika 45. Muda huo ulitosha kwake kuondoka na tuzo ya nyota wa mchezo huo ambao Yanga ilishinda bao 1-0
Pengine huo ni mwanzo wa safari ya Popo kwani kuna uwezekano mkubwa akasajiliwa kama mchezaji wa timu ya vijana ambapo kupitia nafasi hiyo anaweza kutumika katika timu ya wakubwa
Popo anaweza kufuata nyayo za Clement Mzize ambaye pia chimbuko lake kuunganishwa na Yanga ni baada ya Wananchi kumpendekeza kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla