Kiungo mshambuliaji Precious Christopher raia wa Nigeria, amekamilisha usajili wa kujiunga na Yanga Princess akitokea Simba Queens, imefahamika
Precious ni kama amerudi nyumbani kwani kabla ya kujiunga na Simba Queens msimu uliopita, aliitumikia Yanga Princess kwa misimu miwili
Precious amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Yanga Princess wenye kipengele cha kuongeza kama atafanya vizuri
Msimu uliopita Precious aliichezea Simba Queens akifunga mabao mawili na asisti tatu kwenye mechi 18 za Ligi Kuu alizocheza
Wakala wa mchezaji huyo, Abiola Babatunde alisema tayari kiungo huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na sasa ni mchezaji halali wa wana jangwani
“Yanga ni kama nyubani na kwa mara ya kwanza alijulikana Tanzania baada ya kucheza hapa, kaamua kurejea baada ya mkataba wake na Simba kumalizika,” alisema Babatunde