Yanga na washambuliaji wa Congo ni 'damdam'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Aug 2025
Yanga na washambuliaji wa Congo ni 'damdam'

Klabu ya Yanga imeendelea kuonesha imani kwa washambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo), na si kwa bahati tu, historia imewapa sababu ya kuamini.

Katika misimu ya karibuni, majina kama Heritier Makambo, Fiston Mayele na Jean Baleke wamepita Yanga huku Makambo na Mayele wakiacha alama isiyofutika Jangwani. Sasa, jina jipya linaingia kwenye ukurasa huo, Andy Boyeli.

Makambo: Mwanzo wa Simulizi ya Kongo Jangwani

Msimu wa 2018/19, Yanga ilifanya usajili ambao wengi hawakuuona kama tishio, Heritier Makambo. Alipowasili, hakuwahi kujulikana sana, lakini chini ya kocha Mwinyi Zahera, Makambo aligeuka kuwa nguzo muhimu ya ushambuliaji wa Yanga.

Alifunga mabao 18, akaiweka Yanga katika nafasi ya pili licha ya hali mbaya ya kiuchumi iliyokuwa ikiikumba klabu.

Mafanikio hayo yalimrudisha Makambo msimu wa 2021/22, lakini safari yake ya pili haikuwa ya kung'ara kama ile ya kwanza. Alikutana na ushindani mkali kutoka kwa mchezaji mwingine wa DR Congo, Fiston Mayele, ambaye kwa hakika aliibadilisha historia ya washambuliaji wa kigeni katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mayele: Mkali Aliyechonga Historia

Katika misimu miwili aliyohudumu Yanga, Fiston Mayele alikuwa si tu mshambuliaji, bali nembo ya ushindi. Alifunga zaidi ya mabao 50, akitwaa tuzo ya mfungaji bora pamoja na MVP ya ligi.

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF, Mayele aliibuka mfungaji bora kwa mabao 7 na kuipeleka Yanga hadi fainal, rekodi isiyopaswa kupuuzwa.

Mayele aliinua hadhi ya wachezaji wa DR Congo ndani ya Yanga, na akaweka kiwango ambacho washambuliaji wote watakaokuja baada yake watapimwa nacho.

Boyeli: Mrithi Mwenye Mzigo Mkubwa

Katika dirisha hili la usajili, Yanga imeamua kuendeleza imani hiyo kwa kumsajili Andy Boyeli. Alitamba akiwa na Power Dynamos ya Zambia, ambapo msimu wa 2023/24 alifunga mabao 18 na kuwa mfungaji bora na MVP wa ligi hiyo.

Msimu uliofuata, alisajiliwa na Shekhukhune United ya Afrika Kusini, ambako alifunga mabao 7 katika mechi 25, rekodi ya wastani lakini ya kuonyesha anaweza kupambana katika ligi ngumu.

Boyeli ni mshambuliaji wa kati aina ya wachezaji wanaoishi ndani ya boksi. Tofauti na Clement Mzize au Prince Dube ambao hupenda kuhama hama eneo la ushambuliaji, Boyeli ni target man halisi, anayesubiri nafasi ili aumize.

Je, Ataweza Kupita Njia za Makambo na Mayele?

Boyeli anakutana na changamoto ya kupimwa dhidi ya historia ya mafanikio ya wenzake kutoka DR Congo. Mashabiki wa Yanga tayari wana matarajio makubwa, wakimlinganisha na Makambo aliyewahi kuwa shujaa wao, na zaidi na Mayele, aliyeacha pengo kubwa la kiufundi na kihisia.

Lakini pia, historia iko upande wake. Wachezaji wa DR Congo wamekuwa na "chemistry" ya kipekee na mfumo wa Yanga, na kama Boyeli ataweza kujipambanua kwa kutumia nguvu, nafasi, na weledi wake wa kufunga, ana kila sababu ya kuandika historia yake binafsi.

Kuingia kwa Boyeli si tu kuongeza nguvu katika kikosi cha Yanga, bali ni mwendelezo wa simulizi ya mafanikio ya wakali kutoka DR Congo ndani ya Jangwani. Kama ilivyokuwa kwa Makambo, Mayele na hata kina Nonda Shaban wa miaka ya zamani, mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu kuona kama Boyeli ndiye sura mpya ya hofu kwa mabeki wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’