Wakati sherehe kubwa ikitarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk John Magufuli kukabidhi taji la ubingwa wa VPL kwa mabingwa wapya msimu huu Simba, sherehe ambayo pia itahudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda pamoja na vongozi wengine waandamizi wa Serikali, mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu, Yanga watakuwa mkoani Shinyanga wakipepetana na Mwadui FC.
Wachezaji 20 na viongozi nane wa Yanga walitua mapema jana mkoani Shinyanga tayari kwa mchezo huo unaotarajia kuanza saa kumi kamili jioni.
Yanga itakuwa na kibarua cha kuhakikisha inaibuka na ushindi kwenye mchezo huo ili kuondokana na rekodi mbaya ya kutopata ushindi katika michezo nane iliyopita.
Yanga imeenda Shinyanga bila ya kocha wake Mkuu Mwinyi Zahera ambaye amerejea kwao DR Congo kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Nigeria.
Mapema jana Zahera alisaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha Yanga hivyo kufuta uzushi uliosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa kocha huyo alikuwa 'amekimbia ukata'.
Kwa sasa kikosi cha Yanga kiko chini ya makocha Noel Mwandila na Shedrack Nsajigwa.

ADVERTISE HERE