Yanga imemtambulisha kiungo mshambuliaji Ecua Celestin ambaye ametua akitokea klabu ya Asec Mimosas aliyoitumikia msimu uliopita kwa mkopo kutoka Zoman Fc
Ecua ndiye mchezaji bora wa ligi kuu ya Ivory Coast (MVP) akihusika katika mabao 27, msimu uliopita akifunga 15 na kutoa asisti 12
Ni mchezaji aliyekamilika kwelikweli kwani anaweza kutumika katika eneo lolote kwenye safu ya ushambuliaji kuanzia namba 7, 8, 9, 10 na 11
Anafunga, anatoa pasi za mabao, ana kasi, nguvu na maarifa ya ziada akitumia guu lake la kushoto
Katika dirisha hili Yanga imesajili watu wa kazi kwelikweli, ni usajili ambao umelenga michuano ya Kimataifa zaidi hivyo ni wazi hapa ndani vipigo vitatembea sana
Sifa nyingine ya kipekee kwa Acua ni umahiri wake katika kupiga mikwaju ya penati. Unaweza kusema sasa Yanga imepata mtaalam wa kubadili penati kuwa mabao
Msimu uliopita Stephane Aziz Ki ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kupiga penati, Pacome akachukua majukumu baada ya Aziz Ki kuondoka na sasa mtaalam mwingine ametua
Licha ya ofa nyingi kutua mezani kwake, Acua alichagua kujiunga na Yanga, akiamini ndio timu sahihi kwake
Yanga ina historia na ma-MVP wa Ivory Coast, alikuja Aziz Ki, Pacome na sasa Ecua