Baada ya kutangaza kuachana na Simba, zilisikika kauli nyingi huko mitandaoni ooh..hana majabu..mara kazeeka...! lakini ukweli Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' bado yuko katika nyakati bora za maisha yake kama mchezaji
Akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya CHAN 2024 dhidi ya Burkina Faso, Zimbwe Jr alidhihirisha bado sana hajamalizana na mpira wa miguu
Kwa mujibu wa takwimu, Zimbwe Jr ambaye alifunga bao la pili la Stars katika ushindi wa mabao 2-0, alikuwa na mchango mkubwa katika mchezo huo
Alitoa pasi muhimu 4 huku akitengeneza nafasi moja na akifunga goli pia. Alipiga pasi sahihi 52, akiondoa mipira miwili ya hatari na kuingilia mipira minne
Bila shaka mabosi wa Yanga jana walifuatilia mchezo wa Stars dhidi ya Burkina Faso wakiwa na nyuso za tabasamu kutokana na kile walichokiona kutoka kwa Zimbwe Jr
