Yanga yaongeza tisa kikosini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Aug 2025
Yanga yaongeza tisa kikosini

Utambulisho wa Mohamed Doumbia jana umehitimisha nyota wa kigeni waliosajiliwa na Yanga katika dirisha hili la usajili

Yanga imeongeza wachezaji watano wa kigeni ambao ni Moussa Balla Conte, Andy Boyeli, Lassine Kouma, Ecua Celestin na Doumbia

Kwa upande wa wachezaji wa ndani waliotambulishwa mpaka sasa ni Offen Chikola, Aboubakar Nidhar Othman 'Ninju' na Mohamed Abdallah 'Casemiro'

Bado Yanga haijamaliza kutambulisha ambapo inaweza ikafunga dirisha hili kwa utambulisho wa beki wa kushoto, Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' aliyekuwa nahodha wa Simba

Yanga ilishakamilisha usajili wa Zimbwe Jr ambaye juzi aling'ara katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya CHAN akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dhidi ya Burkina Faso akifunga bao katika ushindi wa mabao 2-0

Katika dirisha hili Yanga imefunga hesabu zake ikiwa imeongeza wachezaji tisa kikosini

Wachezaji walioondoka ni Kennedy Musonda, Clatous Chama, Stephane Aziz Ki, Khalid Aucho na Jonathan Ikangalombo ambaye yuko kwenye majadiliano ya uongozi wa Yanga ili atolewe kwa mkopo au mkataba wake uvunjwe

Upande wa wachezaji wa ndani Yanga ikithibitisha kuondoka kwa Jonas Mkude anayetajwa kujiunga na klabu ya Singida Black Stars

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’