Zahera ataipa mafanikio Yanga, apewe muda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 May 2018
Zahera ataipa mafanikio Yanga, apewe muda
Jana Yanga imemalizana na kocha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mwinyi Zahera ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga.

Zahera hakusaini mkataba mara moja alipowasili mwezi uliopita kukiwa na taarifa kwamba kulikuwa na makubaliano baina yake na uongozi wa Yanga ili apate muda wa kukiangalia kikosi pia uongozi ukitaka kupima uwezo wake.

Hatimaye jana ameweza kusaini mkataba wa miaka miwili kisha kurejea Congo kwa majukumu ya kikosi cha timu ya Taifa inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Nigeria.

Licha ya kusaini mkataba wa kuifundisha Yanga, Zahera ataendelea na majukumu yake ya kocha msaidizi wa DR Congo.

Kwa siku chache alizokaa na kikosi cha Yanga, kocha huyo ameonyesha anao uwezo wa kuwarejeshea heshima mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania.

Zahera tayari amewasilisha mpango wake wa namna anavyotaka kuitengeneza Yanga kwa viongozi wa klabu hiyo na sasa yapaswa apewe ushirikiano.

Wale wanaohoji uwezo wake wasubiri watauona.

Waliofuatilia kwa makini mchezo wa Yanga dhidi ya Rayon Sports, watakubaliana nami kuwa kuna vitu tayari vimeanza kuonekana katika kikosi cha Yanga.

Zahera ameanza kutengeneza timu inayotumia filosofia ya kushambulia kwa kasi pia kujilinda pamoja 'total football'. Kinachokosekana kwa sasa ni wachezaji sahihi wa kwendana na mfumo.

Naamini akiachwa asajili wachezaji anaowataka na kuruhusiwa kufanya mabadiliko yote kadiri aonavyo inafaa, Yanga itakuwa moto wa kuotea mbali.

Zahera amecheza soka Ulaya kwa miaka mingi, pia sio jambo dogo kuteuliwa kuwa kocha Msaidizi wa DR Congo kama CV yako ni ya kutilia shaka.

Congo wametuacha mbali sana kwenye viwango vya soka ngazi ya vilabu na hata timu ya Taifa.

Jambo la msingi kwa Yanga sasa ni kwamba timu inakocha baada ya kuondoka kwa George Lwandamina.

Hatma ya Nsajigwa na Mwandila sasa itakuwa mikononi mwa kocha. Ni uamuzi wake kuamua kuendelea nao au kupendekeza wengine.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
11h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
15h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
16h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
16h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’