Bado ushindi umekuwa mgumu kwa kikosi cha Yanga baada ya leo kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC mkoani Shinyanga.
Shuti la mbali ya Aly Awesu alilopiga kwenye dakika ya 19 liliipa Mwadui FC bao pekee la ushindi kwenye mchezo huo.
Huo unakuwa mchezo wa tisa mfululizo kwa kikosi cha Yanga kuondoka dimbani bila ya alama tatu.
Mara ya mwisho Yanga kupata ushindi ilikuwa April 07 2018 ilipoilaza Wolaita Dicha mabao 2-0 kwenye uwanja wa Taifa.
Aidha makocha Noel Mwandila na Shedrack Nsajigwa wamekuwa na mkosi kwani tangu kuondoka kwa Lwandamina wameiongoza Yanga katika michezo yote hiyo bila ushindi

ADVERTISE HERE