Yanga kuifuata Rayon Sports Jumatano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Aug 2025
Yanga kuifuata Rayon Sports Jumatano

Kikosi cha Yanga, Jumatano August 13 kitaelekea Rwanda tayari kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports ambao utapigwa Ijumaa, August 15 katika uwanja wa Amahoro

Yanga imealikwa na Rayon Sports kwenye shamrashamra za Rayon Day, tamasha maalum la kukaribisha msimu mpya

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha mkakati huo wa Wananchi kuelekea Rwanda siku ya Jumatano huku akiwataka wale wanaotaka kusafiri kuandaa utaratibu wa safari na kuwasilisha taarifa zao kwa uongozi

Baada ya mchezo dhidi ya Rayon Sports, huenda Yanga ikaelekea Misri kuhitimisha wiki mbili za maandalizi yake

Kamwe amesema watatoa taarifa juu ya mipango hiyo ya pre-season baada ya mchezo dhidi ya Rayon

"Mpaka sasa kikosi chetu kinaendelea na program za mazoezi KMC Complex, siku ya Jumatano tutasafiri kuelekea Rwanda kwa ajili ya mchezo dhidi ya Rayon Sports"

"Kuhusu wapi tutaelekea baada ya mchezo dhidi ya Rayon, tutatoa taarifa baada ya mchezo huo," alisema Kamwe

Inaelezwa Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz amependekeza kikosi chake kuelekea Misri kuhitimisha wiki mbili za maandalizi kabla ya kurejea nchini tayari kwa Wiki ya Mwananchi ambayo kilele chake kitakuwa wiki ya kwanza ya mwezi Septemba 2025

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
28m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’