Yanga yapaa Rwanda, Folz aahidi burudani kwa Wananchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Aug 2025
Yanga yapaa Rwanda, Folz aahidi burudani kwa Wananchi

Kikosi cha Yanga kimeondoka jijini Dar es salaam jioni ya leo Jumatano kuelekea Rwanda tayari kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports utakaopigwa Ijumaa, August 15

Msafara uliojumuisha wachezaji 24 umeelekea Rwanda huku mkufunzi wa timu hiyo, Romain Folz akiwa na matumaini makubwa kuelekea mchezo huo

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuondoka JNIA, Folz alisema muda mchache aliopata kuiandaa timu hiyo ameutumia kuwaunganisha nyota wapya na wale wa zamani akiamini watakuwa tayari kucheza mechi ya ushindani siku ya Ijumaa

"Nimefurahishwa na juhudi za wachezaji wangu katika muda mfupi ambao tumefanya maandalizi kabla ya mchezo. Timu yetu ina wachezaji wapya hivyo kwanza tumefanya kazi ya kuwaunganisha na wenzao waliopo"

"Kwa ujumla naweza kusema tupo tayari kufanya kwa vitendo kwa kucheza mchezo wa kirafiki wa ushindani na naona nafasi ya kufanya vizuri," alisema Folz

Folz amesema anatambua mashabiki wana matarajio makubwa kwa timu yao hivyo yuko hapa kuhakikisha anatimiza matarajio hayo

Amesema mchezo dhidi ya Rayon una umuhimu kwani atautumia kama sehemu ya maandalizi katika wakati huu wa pre-season, anaamini watapata kipimo sahihi baada ya wiki mbili za mazoezi

"Mchezo wetu Ijumaa ni kwa ajili ya kutuweka tayari kwa kuwaandaa wachezaji kimwili na kimbinu baada ya mazoezi ya muda naamini utakuwa kipimo sahihi kwetu na kila mchezaji atapata nafasi ya kucheza."

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’