Bodi ya Ligi imezifanyia maboresho kanuni za Ngao ya Jamii kuelekea msimu ujao 2025/26
Maboresho hayo yanakwenda kufuta utaratibu wa michuano hiyo kuchezwa kama mashindano ya timu nne na kurejesha utaratibu wa zamani
Ngao ya Jamii sasa itawakutanisha bingwa wa ligi kuu na bingwa wa kombe la Shirikisho la CRDB (FA)
Endapo itatokea bingwa wa ligi kuu ndiye bingwa wa kombe la FA, basi bingwa na ligi na mshindi wa pili watacheza mechi moja ya Ngao ya Jamii
Kwa mabadiliko hayo huenda tutashuhudia mchezo wa Dabi ya Kariakoo mapema kati ya Yanga dhidi ya Simba
Kalenda ya TPLB inaonyesha Ngao ya Jamii itachezwa kati ya Septemba 11-14 mwaka huu
Yanga ndio mabingwa watetezi wa Ngao ya Jamii ambayo waliitwaa msimu uliopita kwa kuichapa Azam Fc mabao 4-1
ADVERTISE HERE