Katika 'kunogesha' Tamasha la RAYON SPORTS DAY, klabu ya Yanga ikiwa nchini Rwanda, leo itatambulisha usajili wa mchezaji mpya
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema nyota huyo ni sehemu ya kikosi ambacho kilitua Rwanda usiku wa juzi, saa 1 usiku wakitarajiwa kushuka dimba la Amahoro kumenyana na Rayon
Winga Edmund John ndiye anayetajwa kusubiri utambulisho baada ya kukamilisha usajili akitokea klabu ya Singida Black Stars
Edmund alisafiri na kikosi cha Yanga Rwanda na pengine leo ataonekana 'mbashara' akiwa kikosini baada ya utambulisho wake
Nyota huyo anatajwa kuchukua nafasi ya mshambuliaji Clement Mzize ambaye anakamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Esperance, mabingwa wa Tunisia
ADVERTISE HERE